Swali: Mtu ambaye anatanguliza mbele mapenzi ya kuipenda pesa juu ya kutoa swadaqah na matendo mema. Je, haya yanapingana na mapenzi ya kumpenda Allaah (´Azza wa Jall)?

Jibu: Linapingana na ukamilifu wa imani:

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ

“Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mkitowacho, basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi.”[1]

وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا

”Wanalisha chakula, pamoja na kukipenda kwake, masikini na mayatima na mateka.”[2]

Ukitoa katika ile mali unayoipenda, basi hiyo ni dalili kweli inayojulisha imani. Kwa sababu umetanguliza mapenzi ya kumpenda Allaah juu ya mapenzi ya kuipenda mali. Mapenzi yako ya kumtii Allaah umeyatanguliza kabla ya mapenzi ya kuipenda mali.

[1] 03:92

[2] 76:08

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (89) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D9%8A%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-08-07-1439.lite__0.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2018