Pengine washerehekeaji maulidi wakalipwa thawabu kwa nia yao nzuri?

Swali: Ni vipi mtu atafahamu maneno ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kwamba katika “Iqtidhwaa´-us-Swiraatah al-Mustaqiym” kwamba mtu anaweza kulipwa thawabu kwa baadhi ya yale anayoyafanya ambayo yanakwenda kinyume na Sunnah. Lakini analipwa kwa sababu ya makusudio yake mazuri.

Jibu: Mimi nimetaja Hadiyth ya mtu ambaye alichinja Udhhiyah kabla ya swalah ya ´iyd na tukataja maneno ya baadhi ya wanachuoni ambao wamesema kwamba ni lazima kufuata licha ya kuwa mtu atakuwa na makusudio mazuri na tumetaja maneno ya Ibn Mas´uud ambaye alisema:

“Ni wangapi wenye kutaka kheri lakini haiwaipatii.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 08/11/2019