Swali: Mimi nina dada anayegombana na mume wake mwenye madhehebu na mfumo wa Suufiyyah. Anampiga, hamuonei wivu na wala hamuamrishi Hijaab. Anamuacha ndugu zake na marafiki zake wampe mkono na kuzungumza naye. Je, Kishari´ah inajuzu kwake kuomba talaka kupitia mahakamani? Unaninasihi nini mimi na yeye?

Jibu: Alipeleke mahakamani. Qaadhiy ataangalia kama anasema kweli au hapana. Kisha atahukumu vile atakavyoona kwa mujibu wa hukumu za Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–16041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020