Swali 117: Baadhi ya vijana wa nchii hii wanaenda katika miji mbalimbali na wanaona kwamba jambo hilo ni faradhi kwa kila mmoja baada ya kupewa fatwa na baadhi ya wanafunzi. Je, kitendo chao hichi ni sahihi?

Jibu: Haijuzu kwao kwenda isipokuwa kwa idhini ya mtawala. Kwa sababu wao ni raia na raia ni lazima kwake kumtii mtawala. Mtawala akiwapa idhini kutakuwa kumebaki vilevile radhi za wazazi wawili. Asisafiri isipokuwa kwa radhi ya baba yake. Kwa sababu alikuja mtu kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamuomba idhini ya kwenda Jihaad akamuuliza: “Je, wazazi wako wako hai?” Akajibu: “Ndio.” Akamwambia: “Kafanye Jihaad nao.” Baadaye akarudi kwa wazazi wake. Hiyo ni dalili inayofahamisha kwamba ni lazima kupatikane idhini ya wazazi wawili baada ya idhini ya mtawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 305
  • Imechapishwa: 20/10/2019