Swali: Je, magoti yanaingia katika viungo visivyotakiwa kuonekana?

Jibu: Ndio. Viungo vya mwanaume visivyotakiwa kuonekana ni kuanzia kwenye kitovu mpaka kwenye magoti. Kitovu na magoti vyote viwili vinaingia katika viungo visivyotakiwa kuonekana. Ni kama Aayah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ

“Enyi walioamini!  Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu hadi vifundoni.”[1]

Visugudi vinaingia kwenye mikono. Vifundo vinaingia kwenye miguu.  Bi maana pamoja na vifundo. Hapa إِلَى maana yake ni  “pamoja”. Bi maana pamoja na vifundo.

[1] 5:6

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-16-2-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2018