Swali: Nimeuza ardhi na tukaafikiana juu ya bei. Pesa nitazilipa baada ya mwaka mmoja. Ni lini napaswa kutoa zakaah juu ya ardhi hii?

Jibu: Mwaka mmoja baada ya kuandika mkataba. Muda unaanza kuhesabiwa pale kunapoandikwa mkataba. Pindi kunapotimia mwaka mmoja wa mkataba ndipo unatakiwa kutoa zakaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2019