Pale ambapo maandamano yanapelekea katika madhara makubwa zaidi


Kwanza ikiwa mtawala ni muislamu na hajatoka katika Uislamu, haijuzu kabisa kumfanya uasi.

Atafanyiwa subira. Madhara ni mengi kuliko kumfanyia subira mbali na kasoro alizonazo.

Ama ikiwa mtawala sio muislamu na waislamu wakawa na uwezo wa kumuondosha na kuweka aliye bora kuliko yeye, watafanya hivyo. Ama ikiwa hawawezi hilo ila mpaka kwa shari, fitina, mauaji au kukosa mji, hili halijuzu. Haijuzu kuzuia madhara kwa kusababisha mabaya zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=bbMpJI16l2g
  • Imechapishwa: 06/09/2020