Swali: Mimi daima huomba ulinzi dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa mbali. Pamoja na hivyo huja na kunitia wasiwasi ndani ya swalah yangu. Ni ipi dawa ya hilo?

Jibu: Dawa ya hilo ni wewe uombe kinga dhidi ya shaytwaan ukiwa na moyo hadhiri. Si kutamka kwa mdomo peke yake. Ataenda mbali nawe – kwa idhini ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
  • Imechapishwa: 01/09/2020