Swali: Kumepokelewa makatazo ya kuomba du´aa kwa kusema:

اللهم اغفر لي إن شئت

“Ee Allaah! Nisamehe ukitaka.”

اللهم ارحمني إن شئت

“Ee Allaah! Nirehemu ukitaka.”

Je, mtu anaweza kulinganisha na kuomba du´aa kwa kusema:

الله يهديك إن شاء الله

“Allaah akuongoze akitaka.”

الله يرحمك إن شاء الله

“Allaah akurehemu akitaka.”?

Jibu: Ndio, mwombee nduguyo uongofu na wala usifanye uvuaji. Unaposema ´Allaah akitaka` ina maana kwamba hauko thabiti na moyo mmoja katika du´aa yako. Kwa hivyo ni lazima uiamulie na uwe na moyo mmoja na wala usifanye uvuaji.   

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 27/12/2020