Ole wako mume kumwacha mke wako kwenda kwa wanawake Hizbiyyaat


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke ambaye ameolewa kwenda katika mihadhara na Darsa bila ya idhini ya mume pamoja na kujua kuwa mume wake anamkataza?

Jibu: Haijuzu kwake kwenda. Lakini ikiwa ni mwanaume mwema na ashukuru (afurahi) kwa hili. Tunamnasihi mwanaume huyu amchukue na kumpelekea katika nyumba ambayo kunafanywa mihadhara na kwenda nae baada ya kumalizika kwamuhadhara. Haijuzu kwake mume kumkataza ilihali naye hamfunzi. Ole wako, ole wako kwenda na mke wako kwa wanawake Hizbiyyaat! Utarudi ukute yeye yuko upande huu na wewe uko upande mwingine.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1524
  • Imechapishwa: 23/02/2018