Nywele za mwanamke kuonekana ndani ya swalah

Swali 242: Mwanamke kukionekana kitu katika nywele zake ndani ya swalah imebatilika swalah yake?

Jibu: Kukionekana kitu kidogo katika nywele na mwili wake hatoirudi swalah yake kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Haya ndio madhehebu ya Abu Haniyfah na Ahmad.

Lakini kukionekana kitu kikubwa katika nywele zake airudi swalah yake ndani ya wakati kwa mtazamo wa wanachuoni wengi, maimamu wane na wengineo. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 94
  • Imechapishwa: 10/08/2019