1008- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote ambaye ataingiza kwenye nywele zake nywele zisizokuwa zake basi si vyengine isipokuwa ameingiza hali ya uongo.”

Ameipokea Ahmad kupitia kwa Mu´aawiyah kwa cheni ya wapokezi iliotangulia. Ina mapokezi mengi yenye kuitolea ushahidi pamoja vilevile na kwa al-Bukhaariy na Muslim.

Ikiwa hii ndio hukumu kwa mwanamke ambaye ameingiza ndani ya nywele zake nywele zisizokuwa zake, ni ipi hukumu kwa mwanamke kuvaa baruka? Ni ipi hukumu kwa yule mtu mwenye kujuzisha kuivaa ima kwa njia isiyofungamana au kwa njia iliofungamana kwa ajili ya kufuata kichwa mchunga baadhi ya madhehebu na pasi na kujali kuwa anapingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh? Kwani Allaah amemwongoza kuona kuwa ni lazima kuzifuata Hadiyth japokuwa zitakuwa zinaenda kinyume na madhehebu yake, sembuse madhehebu ya wengiene. Tunamuomba Allaah atuzidishie uongofu juu ya uongofu na atutunuku elimu na uchaji.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (3/7)
  • Imechapishwa: 13/05/2019