Nyumbani ndio mahali pa kutulizana kwa mwanamke

Swali: Nina kaka yangu hunishauri kwa Aayah hii:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ

“Tulizaneni majumbani mwenu.” (33:33)

Vipi tunaifayia kazi?

Jibu: Maana yake ni kwamba mwanamke hatoki tu kwa ajili ya kutoka. Mwanamke nyumba yake inatakiwa iwe ndio mahali pa kutulizana kwake. Hatakiwi kuonyesha mapambo na kutoka nyumbani. Nyumba ndio mahali pa kutulizana kwake; nyumbani kwake, nyumba ya mume wake, nyumba ya baba yake, nyumba ya mama yake na nyumba ya watoto wake na ndio pahali pa kutulizana kwake. Hatakiwi kutoka nje kwa sababu ya kutaka kubadilisha hali ya hewa ya nyumba au nataka kutoka kwenda hotelini kwa ajili ya kueshi huko. Haijuzu kwake kusema kuwa yuko nyumbani ambapo anaishi kila mwezi na kila wiki na kwamba anaenda hotelini peke yake aeshi huko kwa raha na asiwe na yeyote na kwamba anataka kubadilisha hali ya hewa nyumbani na kuepuka kelele kali zinazomsumbua ili kueshi peke yake hotelini hali ya kustarehe. Kitu kama hicho hakijuzu. Jambo hilo ni khatari kutokana na Hadiyth isemayo:

“Mwanamke anapovua nguo zake katika nyumba isiyokuwa ya mume wake, basi amevunja [sitara] ilioko kati yake yeye na Allaah.”

Dada zangu! Mwanamke mahali pa kutulizana kwake ni nyumbani kwake. Ikibidi kutoka kwa ajili ya mahitaji yake basi atoke katika wakati maalum kisha arudie. Ama kujiruhusu mwenyewe kuondoka nyumbani na kueshi hotelini na mfano wake, jambo hili khatari yake ni kubwa na shari yake ni mbaya. Ni lazima kwa mwanamke amche Allaah juu ya nafsi yake na achunge na apime manufaa na madhara na asidanganyike na chochote. Ni lazima kwake kumcha Allaah. Kwa sababu Allaah amesema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ

“Tulizaneni majumbani mwenu.”

Nyumba ndio mahali pa kutulizana kwa mwanamke. Nyumba ndio njia ya kuficha uchi wake. Allaah afunike nyuchi za wote.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/وَقَرْنَ-فِي-بُيُوتِكُنَّ
  • Imechapishwa: 11/06/2022