Nyujumbe zinazolengesha tarehe ya usiku wa Qadr kupitia ndoto za waja wema

Swali: Katika zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan kunaenezwa nyujumbe mbalimbali kulengeshwa tarehe ya usiku wa Qadr kupitia ndoto za baadhi ya watu wema. Wamesema kuwa jambo hilo limekariri katika miaka iliyotangulia. Ni kipi kidhibiti cha jambo hilo?

Jibu: Ni kana kwamba mtu huyu ameijua elimu ambayo haikujulikana hata na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuujua wala hakuwalengeshea nao watu. Badala yake aliwahimiza kuutafuta katika zile nyusiku za witiri. Yeye mwenyewe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiutafuta. Hakulengesha. Ina maana huyu amekuja baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akaujua? Ni uongo na uzushi sampuli gani huu?

Tahadharini na simu hizi. Zimekuwa mara nyingi zikitumika kama njia ya kueneza Bid´ah, mambo ya ukhurafi na nyujumbe za uongo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/bryhari–1427-10-7.mp3
  • Imechapishwa: 14/05/2020