Nyinyi Ahl-ul-Bid´ah ndio mmewafungulia mlango zanaadiqah wa kuyapotosha maandiko

Wale wenye kuwekea maandiko ya Pepo, Moto, mizani na kufufuliwa Ta´wiyl ni wakanamungu Zanaadiqah. Watu hawa wanapinga kufufuliwa, Pepo, Moto na Njia. Mambo haya wanayapinga na kuyawekea Ta´wiyl. Ibn-ul-Qayyim anasema kuyawekea Ta´wiyl maandiko yanayozungumza juu ya kufufuliwa, Pepo, Moto na mizani ni jambo jepesi kwa mtu mwenye kutaka kucheza na maandiko kuliko kucheza na maandiko yanayozungumzia sifa na ni jarima kubwa kabisa – tunaomba Allaah atukinge. Ni kwa nini mnawaita watu hawa kuwa ni wakanamungu na mnafikia mpaka kuwakufurisha kwa sababu wameyawekea maandiko haya Ta´wiyl na huku mnaona kuwa mna haki ya kufanya hivo? Lakini ni kwa nini wakati huo huo mnajuzisha kufanyia Ta´wiyl dalili za Qur-aan na Sunnah ambazo zinamthibitishia ukamilifu Allaah kama mfano wa elimu, uwezo, utashi, usikizi, uoni, kuwa juu, kulingana na mfano wa hayo! Ni kwa nini mnayawekea Ta´wiyl kisha mnawakemea wakanamungu hawa na isitoshe mnawaita kuwa ni wakanamungu kwa sababu wamewekea Ta´wiyl dalili za Qur-aan na Sunnah zinazozungumzia juu ya kufufuliwa. Ikiwa mnajuzisha kupotosha sifa za Allaah kwa kutumia mfumo huu mchafu, wao pia kadhalika ni sahali zaidi kuliko nyinyi mlivyokuwa na usahali wa kufanyia Ta´wiyl sifa za Allaah. Nyinyi ndio mnawafanya maadui wa Allaah kupinga kufufuliwa, Pepo na Moto na kufunika hilo kwa kutumia Ta´wiyl. Mfumo ni ule ule. Nyote ni wapotoshaji. Ni kwa nini mnawakemea watu hawa na hamjikemei nyinyi wenyewe pamoja na kuwa mnajua ukhatari wa mfumo huu. Huu ni mfumo wa upotoshaji wanaita kuwa ni “Ta´wiyl”. Wakanamungu na wao wanaita kuwa ni Ta´wiyl kama nyinyi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 27/08/2020