Swali: Kipindi cha mwisho kumeenea fatwa inayojuzisha zile nyimbo zinazopigwa katika taarifa za khabari na barnamiji za TV kwa hoja kwamba ni fupi na haziamshi hisia. Unasemaje juu ya fatwa hii?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameharamisha ala za muziki na mafirimbi. Kwa mujibu wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) wanazuoni wameafikiana juu ya hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikataza kitu basi haijuzu kwa yeyote kuvua chochote katika hayo. Haijuzu kufanya hivo. Hakuna katika muziki chochote ambacho ni halali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 22/04/2021