Nyayo za wauaji wa ´Uthmaan bin ´Affaan


Khawaarij walifanya uasi kwa kutumia jina la dini. Khawaarij ambao walimuua kiongozi wa waumini ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) walimuua kwa kutumia jina la dini. Khawaarij ni janga juu ya Uislamu na waislamu. Migomo na milipuko hii ni matendo ya Khawaarij. Uislamu hauna lolote kuhusiana na hayo. Wanawakilisha mfumo wa Khawaarij kwa mfumo wa wauaji wa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na hawawakilishi mfumo wa Qur-aan na Sunnah. Tazama ni vijana wangapi wamedanganyika nao. Wamejiunga na walipuaji. Wamejilipua wao wenyewe na waliokuwa pamoja nao. Wamejiua wao wenyewe na watu wengine wasiokuwa na hatia kwa njia isiyokuwa sahihi na iliyowekwa katika Shari´ah. Allaah hakuteremsha dalili yoyote juu ya hilo. Watoto wa waislamu wengi wamepotea kwa njia kama hii. Ndugu yangu, ndio maana kuwa na mfumo sahihi ni karama kubwa. Ni neema kubwa kwa kule Allaah kukutunukia kuwa na ´Aqiydah na mfumo sahihi. Kufa juu ya Qur-aan na Sunnah. Ishi kutokamana na Qur-aan na Sunnah na ufe – Allaah akitaka – na kufufuliwa kutokaman na Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ath-Thabaat ´alaa as-Swiraat al-Mustaqiym yakuun bil-´Ilm http://olamayemen.com/Dars-9998
  • Imechapishwa: 06/05/2018