Nuru mbili tofauti za Allaah


Swali: Je, ni sahihi kusema kuwa Aayah:

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi.” (24:35)

maana yake ni kwamba Allaah anaziangaza mbingu na ardhi?

Jibu: Ndio. Kuna nuru aina mbili. Nuru ambayo ni moja katika sifa za Allaah (´Azza wa Jall) na haikuumbwa. Ni moja katika sifa za Allaah. Nuru nyingine imeumbwa. Ni kama mfano wa nuru ya jua, nuru ya mwezi, nuru ya nyota, umeme na kadhalika. Hizi ni nuru zilizoumbwa. Allaah ndiye ambaye kaziumba. Allaah ndiye ambaye kaiangaza mbingu na ardhi kwa viumbe hivi. Mfano wa nuru ya Allaah ambayo ni sifa Yake imetajwa katika maneno Yake (Ta´ala):

وَأَشْرَقَتِ الْأَرْضُ بِنُورِ رَبِّهَا وَوُضِعَ الْكِتَابُ وَجِيءَ بِالنَّبِيِّينَ وَالشُّهَدَاءِ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

“Na ardhi itang’ara kwa Nuru ya Mola wake na Kitabu [cha ‘amali] kitawekwa na wataletwa Manabii na Mashahidi, na itakidhiwa baina yao kwa haki – nao hawatodhulumiwa.” (39:69)

Pindi Allaah atapokuja siku ya Qiyaamah kwa ajili ya kuwahukumu waja Wake ardhi itang´ara kwa ajili ya nuru Yake (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1434-08-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/05/2018