Nuru iliyoumbwa na ambayo haikuumbwa

Swali: Namwomba Shaykh anifasirie maneno ya Allaah (Ta´ala):

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi.”[1]?

Jibu: Maana ya Aayah tukufu kwa mujibu wa wanachuoni ni kwamba Allaah (Subhaanah) ndiye mwenye kuviangaza. Nuru zote zilizoko mbinguni, ardhini na siku ya Qiyaamah zote zinatokana na nuru ya Allaah (Subhaanah). Zipo nuru aina mbili:

1- Nuru iliyoumbwa. Nayo ni ile ilioko ulimwenguni, Aakhirah, Peponi na kati ya watu hivi sasa yenye kutoka katika nuru ya jua, mwezi na nyota. Vivyo hivyo nuru ya umeme na moto. Zote hizi zimeumbwa. Ni katika viumbe Wake.

2- Nuru ambayo haikuumbwa, bali ni katika sifa Zake (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah (Subhaanah) kwa himdi na sifa Zake zote ndiye Muumbaji na vyengine vyote vimeumbwa. Nuru ya uso Wake na nuru ya dhati Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) vyote havikuumbwa. Bali ni sifa miongoni mwa sifa Zake (Jalla wa ´Alaa). Nuru hii tukufu ni sifa Yake ambayo haikuumbwa. Bali ni sifa miongoni mwa sifa Zake. Ni kama mfano wa usikizi, uoni, mkono, nyayo na sifa Zake nyenginezo tukufu. Hii ndio haki ambayo wamepita kwayo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

[1] 24:35

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/68)
  • Imechapishwa: 09/12/2020