Swali: Swali hili limekariri mara nyingi: ni ipi hukumu ya kufanya picha kwa kutumia video camera? Je, inajuzu kuangalia mkanda wa video ulio na mihadhara, Siyrah ya Mujaahiduun na kadhalika?

Jibu: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikhusisha picha? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kwa jumla:

“Kila mtengeneza picha ni Motoni.”

Haijalishi kitu ikiwa picha itatengenzwa kwa video camera au kifaa kingine. Hadiyth hii inahusu aina zote za picha na kwa malengo yote. Isipokuwa tu mambo ya dharurah. Kwa mfano kupiga picha kwa ajili ya kitambulisho, leseni ya kuendesha n.k. Haya ni mambo ya dharurah na yameruhusiwa kwa ajili ya dharurah.

Kuhusiana na kurekodi kwa ajili ya kuangalia muhadhara, unaweza kustafidi na elimu bila ya njia ya kurekodi video. Unaweza kustafidi na elimu kwa njia ya vitabu, kusikiliza mihadhara yenye kurekodiwa kwa njia ya sauti, kwa njia ya mtu mwenyewe kuhudhuria [sehemu palipo muhadhara]. Jambo hili halikufungamana peke yake kwenye mapicha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_10.mp3
  • Imechapishwa: 23/06/2018