Swali: Kila ni mtu ambaye nahifadhi swalah zote za mkusanyiko msikitini. Baadhi ya siku napitwa na swalah ya Fajr. Nimepitwa na siku tatu sijawafikishwa kuihudhuria pamoja na kwamba nalala na nia ya kuamka na nakuwa ni mwenye kusononeka sana pale ambapo siipati swalah ya Fajr. Hili hutokea kwa mwezi mara tatu au mara nne. Nifanye nini?

Jibu: Kinachokupata ni kwamba unatakiwa kuweka alamu. Ikiwa usingizi wako ni mzito basi waombe familia yako wakuamshe. Ikiwa nyumbani hakuna yeyote, waombe ndugu zako wakuamshe kwa njia ya simu. Allaah akijua moyoni mwako kwamba una maazimio ya kweli ya kutekeleza swalah ya Fajr pamoja na mkusanyiko, basi Allaah (´Azza wa Jall) atakusaidia. Kwa sababu Allaah humwelekea mja Wake zaidi kuliko vile mja wake anavyomwelekea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1229
  • Imechapishwa: 12/09/2019