Ayman adh-Dhwawaahiriy amesisitiza Jihaad dhidi ya mpinzani wa karibu inakuja mbele kabla ya Jihaad kwa mpinzani alie mbali zaidi. Aliandika haya katika makala ya gazeti la “al-Mujaahiduun” – mwezi wa nne 1995 – chini ya anwani “Njia ya kwenda Yerusalemu ni kupitia Cairo”. Huko, aliandika wazi kabisa:

“Yerusalemu haitoshinda wala kunusuriwa mpaka vita ishinde Misri na Algeria na Cairo zinusuriwe.”

Unaona jinsi adh-Dhwawaahiriy anavyoonelea na kufikiria kama Sayyid Qutwub wakati alipoifanyia Takfiyr jamii. Ili ipate kuhakikishwa fikira yeye anaonelea kuwa mtu anatakiwa kwanza aanze na maadui wa karibu, yaani Waislamu, ambao anaonelea kuwa ni makafiri. Haya ndio mawazo ya Khawaarij wa zamani. Hata wao waliwafanyia Takfiyr waislamu na wakaanza kuwapiga vita badala ya badala ya washirikina wa asli. Walimfanyia Takfiyr ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh), wakamfanyia uadui dhidi yake na wakamuua. Walimfanyia Takfiyr ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu), wakamfanyia uasi na wakamuua. Na kadhalika…

Usaamah bin Laadin ana fikira moja kama adh-Dhwawaahiriy ambaye alipata fikira zake kutoka kwa Sayyid Qutwub, ambaye na yeye kwa upande wake alipata fikira zake kutoka kwa Khawaarij. Ni jambo lisilowezekana kwa Usaamah kuwa na fikira hii bila ya kutopatikana yeyote hapo kabla aliemuathiri kwa fikira hii na kumshawishi kwamba huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah na Salaf. Kwa hiyo, ndio maana unaona jinsi harakati za leo za Kiislamu wanavyojiita “Jihaadiyyah Salafiyyah”. Hata hivyo, sio Jihaadiyyah wala Salafiyyah. Uongo huu unatokamana ikiwa ni pamoja na Muhammad Suruur, Muhammad Qutwub, Swalaah as-Saawiy na ‘Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq ambaye amefanya msasa wa fikira za Sayyid Qutwub na kusafisha baadhi ya maneno yake na kuyafanya yakaonekana kuwa kama ni ufahamu wa Ahl-us-Sunnah na mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Ndio maana wengi katika watoto wetu wanadanganywa. Kama jinsi Usaamah bin Laadin alivyowadanganya pia vijana wengine wengi wanaojiita “Vijana wa mwamko”. Waliodanganywa ndio (wanakuwa) kafara. Ama kuhusu viongozi, wanaishi katika misingi ya usalama. Wanageuza vazi kulingana na upepo kutokana na kanuni maarufu, potevu na yenye kupotosha:

“Lengo linawepesisha njia.”

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Saalim as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fikr-ut-Takfiyr, uk. 202-204
  • Imechapishwa: 22/04/2015