Njia tatu za kutuliza na kupoza hasira

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

16- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa kuna mtu alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuusie ambapo akamwambia: “Usighadhibike.” Yule mtu akakariri [kuomba kuusiwa] ambapo akamwambia tena: “Usighadhibike.”

Ni ipi dawa ya hasira? Imepokelewa katika Sunnah Hadiyth nyingi kuhusiana na jinsi ya kutibu hasira. Tunazikusanya ifuatavyo:

1- Hasira inatibiwa kwa wudhuu´. Mwenye kukasirika ni jambo limewekwa katika Shari´ah akatawadha.

2- Akikasirika na hali ya kuwa amesimama anatakiwa kukaa. Huku ni katika kutibu athari za hasira. Kwa kuwa huituliza nafsi yake.

3- Ajitahidi kujizuia na badala yake alete maneno ambayo ni mazuri. Hili linamuhusu yule anayeweza kufanya hivo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 254
  • Imechapishwa: 14/05/2020