Swali: Je, inafaa kumlipa kima kikubwa zaidi ambaye amenikopa kwa sababu amenifanyia wema?

Jibu: Ndio, ni vizuri kufanya hivo ikiwa si yeye ambaye amekuwekea sharti hiyo ya nyongeza. Ikiwa amekukopa ili baadaye uje kulipa ziada, inehesabika ni ribaa. Haina neno kuchukua mkopo mzuri kisha ukazidisha wakati wa kulipa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbora wenu ni yule ambaye anayelipa kwa uzuri.”[1]

[1] al-Bukhaariy (2606) na Muslim (1601).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022