Swali: Inajuzu kuswali Witr kwa Tashahhud moja ambapo mtu haketi isipokuwa katika ile Rak´ah ya tatu?

Jibu: Kuna aina mbili za kuswali kwa yule anayetaka kuswali Witr:

Ya kwanza: Akaswali Rak´ah mbili kwanza. Kisha akaswali Witr kwa Rak´ah moja.

Ya pili: Akaswali Rak´ah tatu kwa mpigo na asipambanue kati yake kwa kuketi wala kutoa Tasliym. Kwa sababu yote hayo yamepokelewa kutoka kwa Salaf. Nadhani pia kuwa kuna Hadiyth iliyorufaishwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kuswali tatu [kwa pamoja][1].

[1] Abu Daawuud (1422).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/116-117)
  • Imechapishwa: 17/06/2017