Swali: Amesema (´Azza wa Jall):

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

“Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio waliovuka mipaka.” (23:07)

Je, mvuka mipaka ni yule mwenye kutenda dhambi kubwa? Je, punyeto inazingatiwa ni katika mlango huu?

Jibu: Ndio. Inaingia katika maneno Yake:

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

“Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio waliovuka mipaka.”

Mbali na ndoa na wale waliomilikiwa na mikono ya kiume. Allaah hakuruhusu jimaa isipokuwa kwa sababu hizi mbili:  ndoa na wale waliomilikiwa na mikono ya kiume. Yule mwenye kufanya jimaa kwa njia zengine mbali na hizi huyu ni mwenye kupetuka mipaka:

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

“Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio waliovuka mipaka.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (69) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/12-07-1438i.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2017