Njia kwa Allaah


Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ

“Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni njia za kumkurubia.” (05:35)

Ni yepi makusudio ya njia?

Jibu: Njia ni ukaribu. Tafuteni njia kwa kumtii (Subhaanahu wa Ta´ala). Utiifu ni njia kwa sababu kunakukurubisha kwa Allaah. Njia si yale yanayosemwa na makhurafi; ya kwamba uweke kati yako wewe na Allaah mkati na kati ambaye atakukurubisha mbele ya Allaah na atakuombea. Huu ni uongo, uzushi na ujinga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 30/06/2018