Swali: Salafiyyah ni nini na una maoni gani juu yao?

Jibu: Salafiyyah ni unasibisho wa Salaf. Salaf ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maimamu wa uongofu kutoka katika zile karne tau bora za kwanza (Radhiya Allaahu ´anhum). Watu hawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewashuhudia wema pale aliposema:

“Watu bora ni wa karne yangu, kisha wataofuatia, kisha wataofuatia. Halafu baada ya hapo watakuja watu ushuhuda wa mmoja wao utashinda kiapo chake na kiapo chake kitashinda ushuhuda wake.”

Ameipokea Imaam Ahmad katika “al-Musnad”, al-Bukhaariy na Muslim.

Salafiyyuun ni wingi wa ´Salafiy`. Salafiy ni unasibisho wa Salaf na tumetangulia kutaja maana yake. Ni wale wenye kufuata mfumo wa Salaf katika kufuata Qur-aan na Sunnah na kulingania katika vitu hivyo na kuvitendea kazi. Kwa hayo ndio wakawa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/165-166)
  • Imechapishwa: 23/08/2020