Nini cha kufanya ukitolewa salamu choni?

Swali: Tunataka kujua ni vipi tutajibu salamu kwa ambaye katutolea salamu na sisi tuko sehemu ya kujisaidia?

Jibu: Mosi ni kwamba asitolewe salamu mtu ambaye yuko sehemu ya kujisaidia mpaka pale atapotoka. Lakini tukichukulia kuwa ameshatolewa salamu, katika hali hii hakuna njia ya kuitikia salamu. Kwa kuwa akiashiria hatomuona, na akiitikia kwa kutamka haifia kwake kumuomba Allaah (Ta´ala) sehemu kama hii. Anachotakiwa ni yeye kusubiri; ikiwa rafiki yake bado yupo amrudishie na yeye salamu na la sivyo kumrudishia kutakuwa kumeanguka kwa sababu ametolewa salamu katika hali ambayo hawezi kuitikia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (13)
  • Imechapishwa: 20/08/2017