Nini (الاستشراق) na (المستشرقين)?

Swali: Tunaomba kujua maana ya (الاستشراق) na (المستشرقين) kwa sababu wengi katika waliohudhuria pengine wasifahamu maana yake.

Jibu: Neno (الاستشراق) na (المستشرقين) ni watu katika wakristo, mayahudi na makafiri wengineo. Walijifunza lugha ya mashariki na kiarabu na wakaandika kuhusu Uislamu na dini nyinginezo. Baadhi yao wanaweza kufanya uadilifu na wakazungumza haki ijapo wengi wao hawafanyi uadilifu na wala hawazungumzi haki. Baadhi wanaweza kuzungumza haki katika baadhi ya maeneo kwa lengo la kuwaghuri watu na sambamba na hilo wakapenyeza batili na shari katika maeneo mengine katika wakristo, mayahudi na wengineo kwa sababu ya kuingia kwao mashariki, wakachukua lugha ya mashariki na wakasoma athari za mashariki na ile dini na uongofu waliyomo watu wa mashariki ili wawaondoe nje ya dini yao, wawatie mashaka juu ya dini yao, wawalinganie katika batili, ukristo, Ba´thiyyah, uyahudi, uabudia masanamu na mengineyo. Dogo wawezalo kufanya ni kuwatia mashaka juu ya dini yao. Dogo wawezalo kufanya kutilia mashaka dini hii na matokeo yake wasiwe na uimara kutokana na zile fikira mbovu, mashaka na matendo mabaya waliyoyaweka ndani ya mioyo yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2682//معنى-الاستشراق-المستشرقين