Swali: Kuna kijana ambaye anataka kuoa msichana ambaye hajui kuwa anaswali au hapana. Je, ndoa hii inajuzu na ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni lazima kuthibitisha kwanza jambo hili. Aulizie kwanza, kwa kuwa kumuoa mwanamke ambaye ni kafiri haijuzu. Kwa Kauli Yake (Subhaanah):

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao.” (60:10)

Na mwenye kuacha Swalah anakufuru, kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni hata kama atakuwa anakubali uwajibu wake. Akiacha kwa uvivu na kuzembea anakufuru. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baina ya mtu na Shirki au kufuru ni kuacha Swalah.”

Na kasema tena (´alayhis-Swalaat was-Salaam):

“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, atakayeiacha amekufuru.”

Ikiwa haswali haijuzu kumuoa. Ama akijua kuwa anaswali vizuri, anaweza kumuoa. Kasema Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mwanamke anaolewa kwa mambo mane: “Kwa mali yake, uzuri wake, nasabu yake na Dini yake, basi shikilia (chagua) mwenye sifa za Dini utasalimika.” Kumchagua mwanamke mwenye Dini ni jambo limefaradhishwa. Na katika Dini jambo muhimu na nguzo kubwa ni Swalah inayokuja baada ya Shahaadah mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 15/03/2018