Nimlazimishe mtoto wa miaka 12 kufunga?


Swali: Mimi nina mwana ambaye amefikisha miaka kumi na mbili. Je, nimlazimishe kufunga au kufunga kwake ni kwa khiyari na sio lazima kwake pamoja na kujua ya kwamba huenda asiweze kufunga mwezi mzima?

Jibu: Ikiwa mtoto wako huyo uliyemtaja hajabaleghe basi si lazima kwake kufunga. Lakini ni wajibu kwako kumlazimisha kufunga ikiwa anaweza kufanya hivo ili ajizoweze kama ambavo anaamrishwa swalah anapofikisha miaka kumi na kupigwa kwa ajili ya hiyo swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/181)
  • Imechapishwa: 16/05/2018