Nimfanye nini mke mwenye ulimi mchafu?


Swali: Mke wangu ananiudhi sana kwa maneno yake machafu na nimeshamvumilia sana. Je, talaka ndio suluhu?

Jibu: Talaka ndio kitu cha mwisho. Mvumilie na uwe na subira kwake. Maadamu ni mke wako na heunda ni mama wa watoto wako kuwa na subira kwake. Usikimbilie talaka isipokuwa wakati wa dharurah. Ikiwa huwezi kabisa kubaki naye basi hali ya mwisho ndio iwe talaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14020
  • Imechapishwa: 22/04/2018