Nimemuona mchumba ananyoa ndevu usingizini

Swali: Kuna mwanaume amechumbia mwanamke. Mwanamke huyo akaona usingizini ananyoa ndevu. Akubaliane nae au hapana?

Jibu: Vipi hali yake alipoamka?

Swali: Alipoamka hali yake aliona kuwa ni nzuri, bi maana hakunyoa ndevu zake. Na ni mtu mzuri wa msimamo.

Jibu: Mwanamke huyu aliyeona mwanaume ambaye amemchumbia usingizini kanyoa ndevu na yeye mwanaume katika hali yake ya sasa hakunyoa, hayadhuru aliyoyaona usingizini na wala asikatae kuolewa nae maadamu ni mtu wa msimamo katika dini na tabia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (05 A)
  • Imechapishwa: 21/09/2020