”Nimekuoza msichana wangu – sawa nimekubali” – ndoa imepita?


Swali: Kuna ndugu mmoja aliniuliza kama nimekwishaoa ambapo nikamjibu kuwa sijaoa. Akanambia kwamba amenioza msichana wake ambapo na mimi nikaitikia kuwa nimekubali, tukapeana mkono na nikaweka mkono wangu juu ya mkono wake. Je, ndoa imekamilika? Maneno haya yanapelekea katika kitu gani pamoja na kuzingatia kwamba msichana wake yuko katika nchi ya mbali?

Jibu: Ni lazima kupatikane ridhaa ya mke na kumtajia. Ni lazima vilevile kuwepo kupatikane ushahidi – mashahidi waadilifu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii na mashahidi waadilifu.”

Ndoa isiyokuwa na mashahidi haisihi. Aidha ni lazima kupatikane idhini yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtumzima haozeshwi mpaka atakwe amri wala bikira mpaka atakwe idhini.” Akaulizwa: “Idhini yake inakuweje?” Akasema: “Akinyamaza.”

Kwa hivyo mliyofanya hayatoshi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/93/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AA%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC-%D8%A8%D9%82%D9%88%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AC%D9%84-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D8%AA%D9%83-%D8%A7%D8%A8%D9%86%D8%AA%D9%8A
  • Imechapishwa: 07/12/2019