”Nimekuoza msichana wangu – sawa nimekubali” – ndoa imepita? II

Swali: Kuna ndugu nilimwambia kwamba sijaoa ambapo akanambia kuwa mke wako ni msichana wangu kwa jina fulani. Nikakubali. Alikuweko hapo ndugu mmoja. Je, ndoa imepita khaswa kwa kuzingatia kwamba msichana huyo ni bikira na wala hakumtaka ushauri?

Jibu: Hakutolewi fatwa juu ya masuala haya. Yanahitajia kuzingatiwa na kutazamwa vizuri. Ni lazima wawepo mashahidi wawili waadilifu. Kwa hivyo ni lazima kwa muulizaji aandike swali lake na alikadimishe kwa baraza la kutoa fatwa ili walitazame. Kwani swali hili linahusiana pia na upande wa pili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 04/06/2021