“Nilifanya kitu fulani katika Ujaahiliyyah”

Swali: Kuna wakati nawasikia baadhi ya watu wema wakisema:

“Wakati wangu wa Ujaahiliyyah nilikuwa nikifanya hivi na vile.”

Je, inafaa kunasibisha kitendo hichi na wakati wa Ujaahiliyyah?

Jibu: Ni Jaahiliyyah kwa nisba yake yeye na si kwa nisba ya watu wote. Ni Jaahiliyyah kwa nisba yake yeye. Anachomaanisha ni katika Ujaahiliyyah wake. Iwapo atasema:

“Nilikuwa nafanya hivi na vile katika Ujaahiliyyah wangu.”

ndio sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (06) http://alfawzan.af.org.sa/node/2049
  • Imechapishwa: 11/12/2016