Nikosoe kama nimekosea


Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy amesema:

“Nilisema kumwambia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal: “Mimi ni mwanaume niliyejaribiwa. Nimejaribiwa kutokukueleza. Nitakueleza na nikosoe ikiwa nimekosea. Qur-aan yote, kuanzia mwanzo mpaka mwisho, ni maneno ya Allaah. Hakuna ndani ya Qur-aan kitu kilichoumbwa. Mwenye kusema kuwa imeumbwa au kitu ndani yake kimeumbwa ni kafiri. Yule mwenye kudai kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa ni kafiri Jahmiy.” Akasema: “Sahihi kabisa.”

  • Mhusika: Imaam Abuul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/259)
  • Imechapishwa: 11/06/2017