Swali: Siku hizi na fitina nyingi niwakumbushapo ndugu zangu haki za watawala ninajihisi mgeni sana na watu wengi hunichukia. Ipi nasaha zako kwangu?

Jibu: Bainisha haki na usawa na si lazima watu wawe radhi nawe. Si lazima. Wewe bainisha haki na usahihi kwa watu na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na za watawala na za wengine. Mwenye kukubali Alhamdulillaah, na asiyekubali wewe umesafisha dhimma yako na umesimamisha hoja juu yake. Hatuko kwa ajili ya kuwaridhisha watu na sifa. Tuko kwa ajili ya kumridhisha Allaah (´Azza wa Jall). Kama alivyopokea ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) mama wa waumini kutoka kwa Mtume wa Allaah kuwa kasema:

“Yule mwenye kutaka kuwaridhisha watu kwa kupata hasira za Allaah, basi atapata hasira za Allaah na za watu. Na mwenye kutaka kumridhisha Allaah kwa kupata hasira za watu, basi atapata radhi za Allaah na za watu.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.subulsalam.com/site/audios/alfozan/divers/130.Asalafiya7aqi qatoha-13-6-1433.mp3 Tarehe: 1433-06-13/2012-05-04
  • Imechapishwa: 09/04/2022