“Nikiingia sehemu fulani basi nimemwacha mke wangu”


Swali 893: Mwanaume akisema “talaka ni yenye kunilazimu endapo nitaingia sehemu fulani” halafu baadaye akaingia. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Mwenye kusema “talaka ni yenye kunilazimu endapo nitaingia sehemu fulani” halafu baadaye akaingia kwa kukusudia pasi na kusahau, basi talaka moja imepita. Asipoingia sehemu aliyokusudia hakukupita kitu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 356
  • Imechapishwa: 20/09/2019