Swali: Kuna bwana mmoja ambaye ana msimamo wa dini ambaye kamuoa mwanamke asiyetaka kuvaa mavazi ya Kishari´ah. Amemnasihi mara nyingi na amemvumilia kipindi kirefu. Anataka kumtaliki, lakini kinachomzuia ni kwamba amekwishazaa naye watoto. Afanye nini?

Jibu: Haya yalikuwa mwanzoni. Alikuwa akijua hali yake. Kama ni mwenye kusifika namna hii, basi asingemuoa kabisa au akamuwekea sharti awe mtu wa dini na kwamba anatakiwa kujisitiri. Hili ndilo lililokuwa linamlazimu. Ama baada ya kupatikana mambo hayo na kuzaa naye watoto, basi bora kwake ni yeye kumwacha khaswa kwa kuzingatia hali yake mbaya, anavaa mavazi ya mapambo na anachanganyikana na wanaume. Watoto wakubwa wanaweza kupambanua wenyewe. Kama bado ni wadogo na akaona ni bora wakabaki na mama yao, basi afanye hivo, na kama anaona bora wabaki na baba yao, basi afanye hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=70710&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 10/01/2021