Nifanye mambo gani ili nimuone Mtume usingizini?


Swali: Je, kuna matendo ambayo anaweza kufanya mtu ili aweze kumuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usingizini?

Jibu: Ndugu! Usijikalifishe kutaka kumuona Mtume. Wewe fuata Sunnah za (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hili linakutosheleza. Ukijaaliwa kumuona Mtume ilihali unajua sifa zake ni vizuri, la sivyo sio jambo la lazima. Lililo juu yako ni kutendea kazi Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
  • Imechapishwa: 13/04/2018