Ni zipi nguzo na masharti ya I´tikaaf?

Swali: Ni zipi nguzo na masharti ya I´tikaaf? Inasihi kufanya I´tikaaf bila ya mtu kufunga?

Jibu: Nguzo ya I´tikaaf, ni kama tulivyosema, ni mtu kulazimiana na msikiti kwa ajili ya kumtii na kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall), kujikurubisha Kwake na mtu kupata nafasi ya kumuabudu. Kuhusu masharti yake ni kama masharti ya ´ibaadah zengine ambapo miongoni mwazo ni Uislamu na akili. I´tikaaf inasihi kwa ambaye hajabaleghe, mvulana na msichana. Inasihi kufanya I´tikaaf bila ya swawm. Inasihi kufanya I´tikaaf katika kila msikiti.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/162)
  • Imechapishwa: 16/06/2017