Swali: Ni yepi yanayotakikana na yaliyo wajibu kwa mfungaji?

Jibu: Mfungaji anatakiwa kukithitisha kumtii Allaah na kujiepusha na yale yote yaliyokatazwa. Ni wajibu kwake kuyahifadhi yale mambo ya wajibu na kujiepusha na mambo ya haramu. Anatakiwa aswali vipindi vitano vyote kwa nyakati zake, ajiepushe na kusengenya, uvumi, ghushi, kula ribaa na kila neno au kitendo cha haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyeacha kusema uongo, kuutendea kazi na ujinga basi Allah hana haja yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/361-362)
  • Imechapishwa: 13/06/2017