Swali: Ni yepi makusudio ya baraka ya daku iliyotajwa katika Hadiyth?

Jibu: Makusudio ya baraka ya daku ni ile baraka ya Kishari´ah na baraka ya kimwili.

Kuhusu baraka ya Kishari´ah ni kule mtu kutendea kazi maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ama baraka ya kimwili ni kule kuupa mwili chakula na kuufanya kuwa na nguvu ya kufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/362)
  • Imechapishwa: 13/06/2017