Ni yepi ambayo mwanamke anaweza kumuonyesha mwanamke mwenzie?


Swali: Ni yepi ambayo mwanamke anaweza kumuonyesha mwanamke mwenzie?

Jibu: Yale yaliyotajwa katika maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ

“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, baba zao, baba za waume wao, wana wao wa kiume, wana wa kiume wa waume zao, kaka zao, wana wa kiume wa kaka zao, wana wa kiume wa dada zao, wanawake wao [dada zao wa Kiislamu]… “[1]

Inajuzu kwa mwanamke kuwaonyesha dada zake wa kiislamu peke yake yale maeneo ya mapambo. Wakati ilipoteremka Aayah tukufu maeneo ya mapambo kunajumuisha kichwa na shingo, mikono mpaka kwenye viwiko na miguu mpaka vifundoni. Viungo hivi ndivo ambavo mwanamke anaweza kumuonyesha dada yake wa kiislamu.

Kuhusu wanawake wa kikafiri, msimamo wake juu ya mwanamke wa kiislamu ni kama mfano wa mwanamme. Haijuzu kwa mwanamke wa kiislamu kuonyesha mbele ya mwanamke wa kikafiri isipokuwa tu yale anayoweza kuyaonyesha mbele ya wanamme wa kando naye.

Je, inafaa kwa mwanamke wa kiislamu kumuonyesha mwanamme uso na viganja vyake vya mikono? Wanazuoni wametofautiana. Wako wanaojuzisha hilo na wengine hawajuzishi hilo. Kujengea juu ya jawabu hili ndio kunatoka jawabu kuhusu ni namna gani mwanamke anatakiwa kuonekana mbele ya mwanamke wa kikafiri. Wale wenye kuona kuwa uso na viganja vya mikono ni viungo visivyotakiwa kuonekana basi haifai kwa mwanamke wa kiislamu kumuonyesha mwanamke wa kikafiri uso na viganja vyake vya mikono. Wale wenye kuona kuwa inafaa kwake kufanya hivo, kama ninavoonelea mimi pia, basi inafaa kwake kufanya hivo.

[1] 24:31

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (6) Dakika: 34:08
  • Imechapishwa: 29/06/2021