Swali: Kuna dada ambaye analazimishwa na mume wake kumhudumia mama yake, pamoja na kuwa mwanamke huyo – yaani mama wa mume wake – husababisha matatizo baina ya wanandoa. Na sasa dada muulizaji hawezi kustahamili zaidi ya hayo. Afanye nini?

Jibu: Allaah Awajaze kheri kwa Da´wah na hima mnayoifanya juu ya Uislamu. Na Allaah Awabariki kwa juhudi zenu na Allaah Aunufaishe Uislamu na Waislamu kupitia kwenu. Ama kuhusiana kama ni wajibu, sio wajibu kwa mwanamke huyu kumhudumia mama wa mume wake, khususan ikiwa anaamiliana naye mu´amala mbaya. Ama nasaha zetu, tunamnasihi azidi kusubiri zaidi na zaidi na zaidi ya alivyosubiri. Hakika ya Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu: Hakika ya Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Pengine hayo (ya kutomhudumia) yakapelekea katika mfarakano na matatizo baina ya mume na mke. Tunamnasihi, kwa njia ya nasaha na si kwa njia ya uwajibu, amvumilie na asaidiane nae na amhudumie kwa mipaka atakayoweza. Ama kuhusiana kama ni wajibu, sio wajibu kwake. Ni juu ya mwanamke asimame kwa kufanya yale atakayoweza katika kazi za nyumbani. Kama ilivyo katika Swahiyh, hakika ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakati Faatwimah alipoja na kumshtakia uzito anaoupata kutokana na kazi za nyumbani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumwambia kuwa huu sio wajibu wako. Kinachotakikana na tunachomnasihi awe na ustahamivu na asaidiane na mume wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=242
  • Imechapishwa: 23/02/2018