Swali: Nimenuia kuandika kuhusu baadhi ya makundi potevu na kuyatahadharisha. Lakini hata hivyo makundi hayo bado ni waislamu. Isitoshe kuna wanachuoni wameyasifu. Nachelea wasije kuniombea du´aa mbaya. Ni zipi nasaha zako pamoja na kuzingatia ya kwamba makundi haya yamepinda?

Jibu: Ni wajibu kwako kubainisha haki. Jambo la wajibu kwako kubainisha haki. Ikiwa una uhakika makosa walionayo na upotevu walionao – una uhakika 100% – vilevile una uwezo na elimu ambayo kwayo unaweza kubainisha ni wajibu kwako kufanya hivi:

 وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ

“Wakati alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu [akawaambia:] “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.”” (03:187)

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ

“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja za wazi na mwongozo baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, basi hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.” (02:159)

Haijuzu kuficha elimu midhali uko nayo na una uhakika juu ya upotevu wa baadhi ya mapote. Katika hali hii wabainishie watu kwa minajili watahadhari nayo. Hii ni nasaha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Din ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kwa Allaah, Kitabu chake, Mtume wake, viogozi wa waislamu na watu wa kawaida.”

Usiwaogope watu. Lililo wajibu kwako ni kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Bainisha batili. Radd batili. Usiwaogope watu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 08/12/2017