Ni wajibu kwa mwenye mimba na mnyonyeshaji kulipa masiku yake


Swali: Mwanamke akiacha kufunga miaka ya kufuatana katika Ramadhaan kwa sababu ya mimba au kunyonyesha inafaa kwake kulipa masiku hayo baada ya hapo?

Jibu: Mwanamke akiacha kufunga kwa sababu ya ujauzito au unyonyeshaji, basi ni lazima kwake kuyalipa masiku yake wakati mwingine. Haijalishi kitu hata kama muda umeshakuwa mrefu. Hapati dhambi. Kwa sababu huenda Ramadhaan ya pili ilimjia wakati bado yuko ananyonyesha na hivyo ikawa ni vigumu kwake kufunga. Kwa hivyo tunamwambia asubiri mpaka amalize kunyonyesha na ili asibebe mimba nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/843
  • Imechapishwa: 13/05/2018