Ni wajibu kwa mwanamke mimba kulipa siku alizokula?

Swali: Aliye na mimba akila Ramadhaan. Je, anawajibika kulipa au kulisha tu?

Jibu: Ikiwa alikula kwa kuikhofia nafsi yake, anawajibika kulipa tu. Na ikiwa alikuwa kwa kukhofia mtoto  wake, anawajibika pia kulipa tu. Na ikiwa alikula kwa kukhofia mtoto wake na si kwa kuikhofia nafsi yake, anawajibika kulipa pamoja na kulisha masikini kwa kila siku moja 1,5 kg chakula kinacholiwa sana na watu mahala alipo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020